Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia Wasafi FM, Hans Raphael Mwambeki amesema pesa aliyouzwa mshambuliwa wa Yanga, Fiston Mayele ni kubwa kiasi kwamba Yanga wanaweza kununua wachezaji wazuri kuziba pengo la nyota huyo.
Mayele ambaye ni raia wa Congo anatajwa kumalizana na uongozi wa Yanga baada kuuzwa katika klabu ya Pyramids FC ya nchini Misri kwa kitita cha dola za za Kimarekani milioni 1.2 (sawa na Tsh bilioni 2.8).
"Tsh bilioni 2.8 ni pesa nyingi sana, unaweza kununua kikosi kizima au kuboreshea miundombinu, Yanga wanataka kujenga uwanja pesa kama hizo na nyingine kupitia mashindano mbalimbali ndio za kuanzia.
"Miquissone aliuzwa Tsh bilioni 1.5 kwenda Al Ahly imagine, ni karibu mara mbili ya pesa alizonunuliwa Mayele. Ninaamini viongozi wa Yanga watakuwa smart sana kupitia pesa hizo kupata wachezaji bora wakum-replace Mayele.
"Simba walishindwa kumnunua Manzoki kwa Tsh milioni 400, fikiria kwenye Tsh bilioni 2.8 unapata Manzoki wangapi," amesema Hans.
Iwapo Manzoki alikuwa akiuza kwa tsh milioni 400, kwa pesa walizopata Yanga kwa kumuuza Mayele, ni sawa na wachezai saba wenye thamani ya tsh milioni 400 kila mmoja.