Polisi yaanza uchunguzi tukio la kifo Mbezi Luis



Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limeanza uchunguzi wa tukio la kifo cha Felix Mgeni, anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum linachunguza tukio la kifo cha Mgeni (47), mkazi wa Kimara Temboni, anayedaiwa kuuawa huko maeneo ya Mbezi Luis usiku wa tarehe 14 Julai 2023. Mwili wa marehemu umekutwa kwenye gari aina ya Toyota Rav 4, huku ukiwa na jeraha kubwa kichwani,” amesema Kamanda Muliro.

Kamanda Muliro amesema uchunguzi unaofanyika ni pamoja na, kupeleleza baadhi ya vitu vilivyokutwa eneo la tukio, vingine vikiwa ni vya jinsia ya kike.


“Mwili umehifadhiwa Hospitali ya Mloganzila kwa uchunguzi zaidi na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa baada ya uchunguzi wa kina,” amesema Kamanda Muliro.,

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad