"Kwanza Barnaba kunioa sijaja kwenye maisha yake kwa bahati mbaya tulipitia changamoto nyingi sana, alivyoachana na mama watoto wake nilipambana nae sana, mwaka 2016 - 2017 nikaanza nae akiwa hana chochote nataka watu wafahamu
Nime-hustle na mwanaume wangu tumeanzia chini, Barnaba amekuja kwangu akiwa hana chochote yaani nimeanza nae akiwa hana chochote vyote aliacha kwa mama watoto wake Vitu vyote unavyomuona yuko navyo sasa hivi ni ameanza na mimi
Tumeanza moja nilipitia wakati mgumu sana kwa sababu mwenzangu alishazoea maisha ya familia kwa hiyo alikuwa na strees nyingi sana Lakini nikajitahidi kama mwanamke nilisimama kama mwanamke mpaka leo vile mnavyo muona” - Amesema Raya akihojiwa na chombo kimoja cha habari
Kwa upande wa Mama Kimbo ambaye ni mama yake Raya nae amewataka watu waache kuanza kuichokonoa ndoa ya mwanae ikiwa ni mapema mno