Robertinho Amkataa Bocco Kuwa Meneja wa TIMU, Ataka mtu Kutoka nje ya Nchi

 

Robertinho Amkataa Bocco Kuwa Meneja wa TIMU, Ataka mtu Kutoka nje ya Nchi

Baada ya uongozi wa Simba kuwa kwenye mjadala mzito juu ya kupata meneja mpya wa klabu hiyo, hatimaye Kocha Mkuu wa klabu hiyo raia wa Brazil, Roberto Olivier ‘Robertinho’, ameutaka uongozi kutafuta meneja kutoka nje ya nchi ili kubadili mwenendo wa kikosi hicho.


Kikosi cha Simba kwa sasa kipo kwenye maboresho baada ya kushuhudia ubingwa ukienda kwa watani zao wa jadi Yanga msimu wa 2022/23.


Awali Simba walitaka kumkabidhi mikoba ya Patrick Rweyamamu, Nahodha wao John Bocco, jambo ambalo kocha amepinga na kuwaambia Bocco bado ana nafasi ya kucheza na kama wao wanataka kumpa umeneja sasa ni bora nafasi hiyo wakamkabidhi mgeni.


Hivyo mpango wa Simba kumpa cheo Bocco unaweza ukawa umefika mwisho ikiwa watafikia makubaliano mazuri na mshambuliaji huyo bora wa muda wote anaweza kuendelea kucheza ndani.


Kwa msimu wa 2022/23 Bocco katupia mabao 10 na pasi moja ya bao huku akiwa ametupia hat trick mbili kwenye ligi kinara akiwa ni Fiston Mayele mshambuliaji wa Yanga na Saido Ntibanzokiza wa Simba.


Mastaa wote wawili kuanzia Mayele wa Yanga na Ntibanzokiza wa Simba walitupia mabao 17 kibindoni.


Chanzo chetu kimeeleza kuwa, kwakuwa Simba inataka maboesho makubwa kikosni mwakae, kocha amewashauri watafute kocha meneja kutoka nchi za kizungu au yoyote Afrika mwenye kujua zaidi mambo ya uongozi wa wachezaji ili Bocco aendelee kupata uzoefu wakati akimalizia mpira wake.


“Tunatarajia kuajiri Meneja mzungu, ili aje kurithi mikoba ya Rweyamamu, hii ni baada ya kushauriana kuachna na Bocco ambaye awali ilipangwa yeye ndiye achukue mikoba hiyo,” kilisema Chanzo hicho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad