Rostam Atakiwa Kuthibitisha Tuhuma Dhidi ya Majaji na Mahakimu wa Kisutu Kupokea Maagizo

Rostam Atakiwa Kuthibitisha Tuhuma Dhidi ya Majaji na Mahakimu wa Kisutu Kupokea Maagizo


Chama cha Majaji na Mahakimu Nchini kimeeleza kusikitishwa na Matamshi ya RostamAziz yanayoweza kuhatarisha uhusiano na ushirikiano katika Mihimili ya Dola, hivyo kumtaka athibitishe kauli yake akibainisha Jina la Jaji na lini alipewa maagizo na Kiongozi wa Serikali kutoa maamuzi kinyume na taratibu zilizopo

Mnamo Juni 26, 2023 Rostam Azizi wakati akiongea na Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya Uwekezaji, alinukuliwa akiituhumu aliyoiita Mahakama ya Kisutu kwa kutokuwa huru katika uendeshaji wa shughuli zake

Taarifa ya Chama hicho imesema Uongozi wa Mahakama au Chama Chao haujawahi kupokea tuhuma au lalamiko lolote kutoka kwa Mtu yeyote, ikionyesha Maafisa wa Mahakama kupigiwa simu na kuelekezwa namna ya kutoa maamuzi katika Mahakama hiyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad