Sadio Mane Afukuzwa Bayern Munich

 

Sadio Mane Afukuzwa Bayern Munich

Uongozi wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani umemshauri nyota wao raia wa Senegal, Sadio Mane kuchunguza chaguzi za uhamisho.


Uongozi wa Bayern umethibitisha kwa sasa hauhitaji kumtegemea Msenegali huyo(kwa msimu ujao).


Mane alikuwa ameamua kuendelea na Bayern kabla ya yeye na uongozi wake kupewa taarifa hizo.


Mane ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa katika klabu ya Bayern Munich.


Sadio Mane alijiunga na Bayern msimu wa joto wa 2022, na kusaini kandarasi ya miaka mitatu akitokea Klabu ya Liverpool alikocheza kwa mafanikio makubwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad