Sadio Mane Ampa Makavu Mwandishi, Amchomolea Interview

Sadio Mane Ampa Makavu Mwandishi, Amchomolea Interview


Mshambuliaji wa Bayern Munich Sadio Mane amemkatalia mwandihi wa Habari kufanya nae mahojiano akiwalalamikia kitendo cha kuandikwa vibaya.

Katika moja ya video anasikika mwandishi akimuuliza Sadio Mane;

Mwandishi: Sadio, naweza kukuuliza maswali machache?

Mane: Mnaniua (mnanisema) kila siku na sasa mnataka niongee na nyie?

Baada ya majibu hayo Sadio Mane aliondoka pasipo kufanya mahojiano na Mwandishi huyo.

Sadio Mane ameambiwa atafute Timu kwa kuwa Bayern kwa sasa hawana mipango nae na kitendo hicho kimewafanya Wanahabari kila kukicha kumshambulia Mane wakidai anapokea mshahara mkubwa lakini hana umuhimu katika klabu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad