Mahakama kuu imesitisha uamuzi wa serikali wa kufutilia mbali leseni ya kumiliki silaha ya Jomo Kenyatta mwanawe rais Uhuru Kenyatta na ni baada ya mtoto wa aliyekuwa mkuu wa nchi kuwasilisha ombi la kupinga kuondolewa kwa bunduki yake.
Jomo aliwasilisha ombi chini ya cheti cha dharura akisema kuwa hakufahamishwa sababu za kuzuiwa kwa cheti chake licha ya kuwa na leseni. Mimi na mke wangu tumekuwa tukipokea jumbe za vitisho yaani mtoto huyo alikuwa ameomba mahakama iingilie kati na kukomesha serikali kumpokonya leseni yake ya kumiliki bunduki.
Mwanawe rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, John Jomo Kenyatta aliwasilisha kesi mahakama ya kuu kupinga uamuzi wa serikali kufutilia mbali leseni yake kumiliki bunduki.
John Jomo aliambia Mahakama ya Kikatiba kwamba ana wasiwasi kwamba hatua ya kunyang’anywa leseni yake ya kumiliki bunduki ilikuwa mbinu dhabiti ya Serikali kutumia nguvu za kikatili kumfanya alengwe na wahalifu.
Katika uamuzi wake, Jaji Jairus Ngaah, alizuia Bodi ya Leseni ya Silaha kusitisha kubatilisha bunduki ya Jomo.
“Kwa madhumuni ya kuhifadhi sehemu ndogo ya shauri, likizo iliyotolewa itafanya kazi kama zuio la uamuzi wa mlalamikiwa wa kwanza na wa pili, akitaka kumfutia mwombaji leseni ya silaha au akitaka kusalimisha leseni ya silaha Na. 0000530 au silaha iliyo chini ya leseni hiyo bila kufuata utaratibu unaotazamiwa kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Silaha za Moto, sura ya 1. 114,” yalisomekasoma maagizo ya Ngaah.