Serikali iachane na Familia yangu, Nifuateni Mimi Simnajua Nilipo – Uhuru



RAIS Mstaafu Uhuru Kenyatta amekasirishwa na hatua ya serikali kutuma polisi kufanya msako kwenye makazi ya mwanawe yaliyoko Karen, Nairobi mnamo Ijumaa.

Amesema inasikitisha kwamba serikali inahangaisha wanawe na mamake.

“Tayari ulinzi wa wanangu umeondolewa na hawana silaha za kujilinda. Ikiwa wanapanga kitu chochote kibaya, waniachie wanangu na mamangu. Wanikujie mimi mwenyewe,” amesema Rais Mstaafu Bw Kenyatta.

Ameitaka serikali iangazie kilio cha Wakenya badala ya kuandama wanawe na mamake, Mama Ngina Kenyatta.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad