Serikali ya Uganda Kufunga Tovuti zote za Ngono Kama Tanzania


Serikali ya Uganda imetoa agizo kwa watoa huduma za mtandao kuzuia tovuti za ponografia ili kuwalinda vijana wa taifa hilo kutokana na athari zinazotokana na maudhui hayo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Naibu Spika wa Bunge la Uganda, Thomas Tayebwa kuagiza Serikali kuzuia maudhui yote ya ngono ili kuwalinda vijana wasio na hatia dhidi ya walaghai wa mitandaoni na machapisho ya mitandao ya kijamii yasiyofaa.

"Vijana wetu wanaoneshwa ponografia. Katika nchi za Kiislamu, ponografia imezuiwa. Niambie ni kiasi gani tunaweza kupoteza kama uchumi ikiwa tutazuia tovuti za ponografia nchini. Ponografia inatuua," amesema Tayebwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad