Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, Dkt.Omar Adam amesema haya leo akihojiwa na ZBC kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Sanaa na Filamu na namna wanavyosimamia Mila, Desturi na Utamaduni wa Zanzibar.
"Zanzibar kwa siku moja huwa kuna shughuli 50 hadi 100 hatuwezi kuzuia hilo, hatujapiga marufuku kupiga muziki bali kupiga muziki kwa sauti iliyopitiliza na kucheza muziki kwa mitindo isiyofaa na inayopingana na desturi za Zanzibar hasa huu mtindo wa wakina Dada kucheza kwa kulowesha nguo maji, ni marufuku na Askari wana ruhusa ya kuwakamata” ——— Dkt. Omar Adam.