Serikali Yapiga Marufuku Kucheza na Nguo laini na Kuzilowesha na Maji Kanga Moko



Serikali ya Zanzibar kupitia Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni imepiga marufuku mtindo wa Wanawake kulowesha kwenye maji nguo walizovaa na kisha kucheza nazo mziki kama ambavyo imekua ikifanyia kwenye baadhi ya sherehe ama mikusanyiko.

Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, Dkt.Omar Adam amesema haya leo akihojiwa na ZBC kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Sanaa na Filamu na namna wanavyosimamia Mila, Desturi na Utamaduni wa Zanzibar.

"Zanzibar kwa siku moja huwa kuna shughuli 50 hadi 100 hatuwezi kuzuia hilo, hatujapiga marufuku kupiga muziki bali kupiga muziki kwa sauti iliyopitiliza na kucheza muziki kwa mitindo isiyofaa na inayopingana na desturi za Zanzibar hasa huu mtindo wa wakina Dada kucheza kwa kulowesha nguo maji, ni marufuku na Askari wana ruhusa ya kuwakamata” ——— Dkt. Omar Adam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad