Tafsiri yake ni kwamba wanaopaswa kupewa thamani/hadhi kubwa au kutambulishwa usiku mzito ni wachezaji kutoka nje!
Ukiiangalia kauli hiyo kwa picha kubwa inakupa perception ya mashabiki kwa wachezaji wa nyumbani. Mashabiki wanaamini wachezaji wanaotoka nje ndio wanastahili thamani kubwa na hii imekuwa ikitengenezwa na klabu zetu.
Mimi siamini kwamba kuna mchezaji anatakiwa kutangazwa wa kwanza au wa mwisho, mchana au usiku kwa sababu ya umuhimu/ubora wake.
Kama klabu imesajili wachezaji watano, wakati wa kuwatambulisha haimaanishi atakaekuwa wa kwanza kutambulishwa au wa mwisho au usiku ndio muhimu.
Wachezaji wote wamesajiliwa na klabu, itakapofika muda wa kutambulishwa lazima atakuwepo wa kwanza kutambulishwa na atakuwepo wa mwisho! Kutambulishwa usiku au mchana ni utaratibu tu ambao klabu imeamua kujiwekea lakini haimaanishi anaetambulishwa muda fulani ni bora kuliko atakaetambulishwa muda fulani.
Imejengeka kwenye akili za mashabiki kuwa, mchezaji anaetoka nje ya Tanzania na hawajawahi kumuona sehemu yoyote ndio mchezaji bora.
Kwa mfano sasa hivi Yanga wanamzungumzia mchezaji namba sita [6], akili ya mashabiki wote hawafikirii mchezaji huyo anaweza kuwa mtanzania! Wanafikiria ni mchezaji kutoka mataifa ya Afrika Magharibi.
Mimi nafikiri wachezaji wote wapewe hadhi inayofanana, tuache hiyo kasumba kwamba wachezaji wetu wa nyumbani hawastahili kupewa heshima wanayopewa wachezaji wanaotoka nje