Shafih Dauda "Wachezaji wa Ndani Wamezubaa Hawana Mawakala Wakuwatafutia Timu nje"




Wachezaji wengi wa nyumbani wanasubiri timu za nje ziwatafute, wachezaji wengi wa kigeni wana agency au mawakala ambao wanawatafutia timu!


Wakati mchezaji anapambana uwanjani, wakala anapambana kusambaza CV ya mchezaji kwenye klabu mbalimbali za nchi tofauti.

Kila kitu kinakwenda kwa mpango maalum, hakuna jambo linatokea kwa bahati mbaya. Tanzania ina wachezaji wengi wenye uwezo ziaidi ya Sakho lakini ndio hivyo nani yupo nyuma yao?

Kwa misimu ambayo Simba imecheza michuano ya Afrika mfululizo ni wageni pekee ndio wamefanikiwa kuondoka Simba [Chama, Miquissone, Sakho]. Yanga ameondoka Mayele lakini hakuna mzawa hata mmoja aliyeondoka!

Wachezaji wetu ni kama bado wanacheza msituni, wanacheza huku wakisubiri siku moja ofa nzuri itakuja kutoka klabu kubwa Afrika lakini wachezaji wa kigeni wanacheza huku mawakala wao wakiwa wamewawashia taa ya kuwamulika waonekane. Wanazitafuta fursa kwa ajili ya wachezaji wao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad