Simba huenda ikaachana na mpango wa kumsajili winga Luis Miquissone baada ya kushindwa kufikia nae makubaliano ya mshahara
Kulingana na mwanahabari maarufu wa Ghana Micky Junior, Miquissone ameweka ngumu kupunguza mshahara wake
Al Ahly wako tayari kumuuza au kumtoa kwa mkopo katika timu ambayo itagharamia mashahara wake kwa asilimia 100%
Lakini imeonekana mshahara wake (karibu Mil 95 kwa mwezi) ni tatizo sio kwa Simba tu, klabu nyingi zilizoonyesha nia ya kumuhitaji awali, zimejiondoa
Inaaminika kuwa Miquissone hataki kutolewa kwa mkopo na Al Ahly huku kukiwa hakuna ofa iliyowasilishwa kutaka kumnunua
Winga huyo wa Kimataifa wa Msumbiji, anataka Al Ahly wavunje mkataba wake kama hawataki kuendelea nae ili awe mchezaji huru
Kama Al Ahly watavunja mkataba wao ina maana watamlipa gharama zote na atakuwa huru kufanya mazungumzo mapya na klabu nyingine