Skudu Aweka Rekodi Mchezaji wa Kwanza Kutoka Afrika Kusini Kucheza Ligi kuu ya Tanzania Bara



Mahlatse Makudubela 'Skudu' ameweka rekodi kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika Kusini kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara

Kwa lugha nyingine Yanga inakuwa klabu ya kwanza Tanzania kusajili mchezaji wa ligi kuu ya Afrika Kusini

Ubora na thamani ya ligi ya Afrika Kusini ni kubwa kuliko ligi yetu, Skudu anakwenda kufungua milango kwa wachezaji wengine kutoka Afrika Kusini kuja kucheza Tanzania

Skudu ni mchezaji wa daraja la juu, ni aina ya kiungo mshambuliaji/winga ambaye anaweza kufungua mabeki wagumu

Kama Bernard Morrison alijizolea sifa kwa aina yake ya uchezaji ukiondoa changamoto zake za nje ya uwanja, basi mwalimu wake ni Skudu

Skudu ni mchezaji ambaye hahitaji maneno mengi kumuelezea, wale wenye mashaka nae waweke akiba ya maneno, wamsubiri uwanjani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad