‘Yapo maoni na malalamiko kwamba kifungo cha maisha kiwape nafasi wafungwa nafasi ya kujirekebisha na kulitumikia taifa na kwamba wakati umefika kifungo hiki kiwe na ukomo ili kuwawezesha wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha kuwa na matumaini’amesema Jaji mstaafu.
Aidha ameweka wazi kuwa kuna watu Zaidi ya 600 wanaosubili kunyongwa na hata hivyo wengi wao wanaishi na hofu kubwa kwani wana miaka kadhaa wakingoja adhabu hiyo.
Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande ameyasema hayo alipokuwa akiwakilisha ripoti ya Tume ya Haki Jinai.