Tanzania yashika Nafasi ya 9 kwa Matumizi ya Facebook

 


Mbali na kuwa mtandao maarufu zaidi wa kijamii Duniani huku ukiwa na watumiaji karibu ya Billion 3 kwenye Dunia ya watu Bilioni 8, Unafanya vizuri zaidi kwenye masoko mtandaoni na kuhusu hili hakuna ubishi kuhusu mtandao wa Facebook.


Swali linaweza kuwa je kwenye eneo nililopo kuna watumiaji wa mtandao huu? Basi fahamu kuwa kwa Duniani India ambayo ina watu Bilioni 1.4 ina watumiaji Milioni 314.6 wanaotumia mtandao wa Facebook na kuwafanya kuwa nchi inayooongoza kwa idadi kubwa ya watumiaji wa mtandao huu.


Kwa hapa Afrika msimamo umekaa hivi;


1. Misri (55.7 million)

2. Nigeria (40.3 million)

3. Algeria (31.1 million)

4. Afrika ya Kusini (30.3 million)

5. Morocco (26.9 million)

6. Kenya (13.7 million)

7. Ghana (8.6 million)

8. Tunisia (8.76 million)

9. Tanzania (6.78m)


Nchi ya Tanzania ambayo kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 ina watu zaidi ya Million 61 huku watu Millioni 6.78 ni watumiaji wa mtandao wa Facebook ambayo ni sawa na asilimia 11.1

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad