TANZIA:Ajali yaua Watano Tunduma



Watu watano wamefariki dunia papohapo na wengine kujeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha malori mawili, bajaji na bodaboda katika eneo la Mpakani lililopo Tunduma Wilayani Momba Mkoani Songwe.

Akiongea na @AyoTV_ kwa njia ya simu leo Jumatano July 5, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya amesema ajali hiyo imetokea mchana wa leo “Ni kweli ajali imetokea imesababisha vifo vya Watu watano na majeruhi mpaka sasa wapo 10, ajali imehusisha lori moja la IT, bajaji, bodaboda na lori lingine lililofeli breki"

Kamanda amesema majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Mpakani Tunduma na taarifa kamili itatolewa baadaye “Imetokea majira ya saa sita mchana, bado tunafuatilia chanzo cha ajali hiyo”

Awali akisimulia tukio hilo Shuhuda mmoja amesema “Ilianza IT kumgonga Dereva bodaboda na lori lilikuwa linashuka Dereva bodaboda ameanguka chini lori likamburuza umbali wa kama Mita 20-30, wakati Watu wanashangaa kuna gari imefeli breki ikaburuza Watu wote waliokuwa barabarani na Hiace, Tipa na bajaji na pikipiki kama una Mtu alikuwa anaenda Mpemba au anatoka Mpemba mpigie simu yaani pale kuna Watu kadhaa wamekufa”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad