TETESI: Yanga Wadaiwa Kumshawishi CHAMA Ajiunge Nao, Wakutana nae Kikao cha Siei



CLOTOUS CHOTA CHAMA MWAMBA WA LUSAKA Bado ni mali halali ya Simba Sports Club hadi mwaka 2024 Mwezi july, Viongozi wa Yanga walimtumia Haji Manara kwenda kuongea na Chama pamoja na wasimamizi wa mchezaji ili kuhitaji huduma yake ndani ya kikosi cha Yanga Msimu ujao mazungumzo takribani ya masaa 4 yalifanyika pale Serena Hotel juu ya kumshawishi Chama ajiunge na Yanga msimu ujao.

Offer iliyowekwa mezani kama pesa ya kumsajili na kumshawishi ni dollar 250,000 huku wakimuahidi kumpa mshahara wa milioni 35 yaani 35,000,000 za Kitanzania kila mwezi wawaikilishi wa mchezaji pamoja na mchezaji mwenyewe hawajatoa jibu la ndio au hapana kuanzia siku hiyo hadi leo.

Walichokisema ni kuwa bado tunamkataba na Simba mpaka mwaka kesho kwahiyo tusubiri hadi mazungumzo na Simba yamalizike kisha tutawajibu kama hilo swala linawezekana au haliwezekani kisha mazungumzo yakaishia hapo kilichofata ni kupiga stori kupata kinywaji na kisha kuondoka Chama na wawakilishi wake walitumia Gari aina ya Toyota Hilux double Cabin ya kijivu huku Haji Manara na viongozi aliokuja nao mezanii walitumia Benzi nyeupe ndogo na Toyota Harrie namba E.

Viongozi wa Simba watakaa na CHAMA mara baada ya Simba kuona namna ya kumuongezea mkataba na kuboresha maslahi yake ili aendelee kusalia ndani ya kikosi cha Simba,Kesho Chama anatarajia kuondoka na Jean Baleke pamoja na Che Fondho Malone kuelekea UTURUKI kuungana na wenzake kwenye preseason, Chama bado ni mchezaji halali wa Simba mpaka sasa na hayo yanayoendelea juu yake ni tetesi tu ambazo ni za kawaida kwenye medani ya soka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad