Tetesi za Chama Kwenda Yanga Zawaumiza Kichwa SIMBA, Ahmed Ally Afunguka Chama Bado ni wao


Tetesi za Chama Kwenda Yanga Zawaumiza Kichwa SIMBA,  Ahmed Ally Afunguka Chama Bado ni wao


Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC Ahmed Ally ametolea ufafanuzi taarifa za Mkali wa soka Clatous Chama Raia wa Zambia kudaiwa kuwa amegoma kwenda Uturuki Pre Season na Club hiyo kwasababu anadai stahiki zake.


Kupitia fununu hizo wengine walidai @realclatouschama ana ofa mkononi na anataka kuondoka Simba SC lakini Ahmed Ally ameweka wazi kuwa Club hiyo haina ofa yoyote iliyopokea.


“Kumekua na sintofahamu kuhusu mkataba wa Mwamba wa Lusaka kiasi cha kuzua taharuki miongoni mwa Mashabiki wetu, taarifa ni kwamba Chama bado ana mkataba na Simba kwa muda wa mwaka mmoja hadi mwaka 2024 hatujapokea ofa kutoka klabu yeyote ikihitaji kumnunua Chama na wala hatujapokea maombi ya Mchezaji kutaka kuvunja mkataba”


“Mchezaji yeyote ambaye tunamuhitaji atabaki kuitumikia Simba kulingana na mahitaji ya mkataba wetu” ——— @ahmedally_

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad