Klabu ya Pyramids ipo kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Yanga SC, Fiston Mayele kwa ajili kumsajili kinara huyo wa magoli wa kombe la Shirikisho Afrika 2022/23.
Miamba hiyo ya Misri tayari imefikia makubaliano ya maslahi binafsi na Mayele (29) raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wakati huo huo klabu ya Yanga ipo katika jitihada za kuandaa maisha bila Mayele na tayari ina majina kadhaa mezani ya mshambuliaji ambaye anaweza kuvaa viatu vya kinara huyo wa magoli kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita.
Baadhi ya washambuliaji wanaopigiwa upatu kumrithi Mayele ni Makabi Lilepo (25) raia wa DRC kutoka Al Hilal ya Sudan na Sankara Karamoko (19) raia wa lvory Coast kutoka klabu ya Asec Mimosas.
Je, ni mshambuliaji yupi ambaye unadhani viatu vya Mayele vitamtosha kati ya Lilepo na Karamoko ndugu msomaji?