Treni za Kisasa Zilizochongoka Zipo?, Kwa mara ya kwanza Korea watoa Majibu kwa Watanzania



Muonekano wa maendeleo ya utengenezaji wa moja kati ya seti 10 za treni za Kisasa (EMU) kwa ajili Reli ya kisasa (SGR), zinazotengenezwa na kampuni ya Hyundai Rotem ya Korea ya Kusini, ambapo kazi za utandazaji wa nyaya za umeme, mfumo wa usambazaji hewa ndani ya treni na ufungaji wa vifaa vya kielektroniki zinaendelea.

Kampuni hiyo ilipewa zabuni na Serikali ya Tanzania ya kutengeneza vichwa 17 vya treni vya umeme na seti 10 za treni za kisasa EMU.

Pamoja na kazi za utengenezaji wa treni hizo za kisasa, Hyundai Rotem kwa kushirikiana na Wataalam kutoka TRC wanaendelea na majaribio ya mifumo mbalimbali katika vichwa vya treni vya umeme, mjini Changwon, Korea ya Kusini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad