Tshabalala Afunguka Madai ya Kutumia Ushirikina

Tshabalala Afunguka Madai ya Kutumia Ushirikina


Beki wa kushoto wa Simba SC, Mohamed Hussein 'Tshabalala' amefungukia madai ya kuwa anatumia ushirikina ili kuweza kucheza kwa muda mrefu na kusema hizo ni fikra potofu kwa baadhi ya watu.


Tshabalala ameyasema hayo kupitia mahojiano aliyoyafanya na Azam TV ambapo amesema, watu wanaopenda kuchukulia mafanikio ya wenzao kwa mtazamo hasi ni wazito wa kufikiri.


“Watu waache kufikiria watu kwenye dhana potofu, wakiona tu unacheza wanadhani mambo yanatokea tu kirahisi. Hawajui kuna miiko ya mpira, kuna vitu mtu unajizuia ili uweze kujitunza, usiwe na injury za mara kwa mara na mambo mengine," alisema Tshabalala.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad