Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere Kuanza Kufanya Kazi Juni Mwakani



Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere Kuanza Kufanya Kazi Juni Mwakani

Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere unatarajiwa kukamilika Juni, mwakani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amewaambia wahariri wa habari leo Alhamisi, Julai 2023 kuwa mradi huo kwa sasa umefika asilimia 90.

Kwa mujibu wa Chande, kukamilika kwa bwawa hilo kutaongeza ufanisi na changamoto ya umeme nchini itabaki kuwa historia.

Chande amesema ujenzi wa bwawa hilo litakalozalisha megawat 2100 umetumia kiasi cha Sh6.5 trioni fedha ambazo ni nyingi kuliko miradi yote nchini zilizotolewa na Serikali.

“Ujenzi wa bwawa hili ukikamilika tutakuwa na uwezo wa kuunganisha wateja wa nyumba zote nchini, “ amesema Chande na kuongeza kuwa kwa matumizia ya sasa ni megawati 1400 pekee.

Amesema asilimia 50 kwa sasa ni wateja wa majumbani na iliyobaki inatumiwa na wateja wakuwa wa viwanda.

Naye Mwenyekiti wa Juiwaa la wahariri (TEF ), Deodatus Balile amelipongeza shirika hilo kwa maboresho wanayoendelea kufanya katika utoaji wa huduma zake kwa wateja na ameshauri mfumo wa utendaji wa shirika hilo utumike pia katika taasisi zingine za umma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad