Ujumbe wa Diamond Kwa Mama yake 'Nilikwambia Kwenye Dadala ipo SIKU nitatoboa kupitia muziki'

 

Ujumbe wa Diamond Kwa Mama yake 'Nilikwambia Kwenye Dadala ipo SIKU nitatoboa kupitia muziki'

Ikiwa ni kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa, mama mzazi wa staa wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, Staa huyo jana alimuandikia ujumbe huu mama yake Mzazi kwa Mutakia Siku Njema ya Kuzaliwa


"Nakumbuka Mwaka Mmoja wakati unafanya kazi ya Saloon kariakoo, tukiwa tunarudi usiku majira kama ya saa sita hivi kwenye Daladala nikakwambia


"Usijali mama Kuna siku nitatoboa kwenye mziki na nitakufungulia na wewe Saloon yako. Vyote naweza visahau lakini maneno haya siwezi yasahau, kwa sababu nilikuambia kwa uchungu nilipokuona unanitazama kwa huruma na Uchungu.


"Kwa jinsi nilivyokua nahangaika na maumivu ya kiti chamoto kwenye Daladala ya Hiace. Nakupenda na Nakuheshimu sana na siku zote ujue kwamba wewe ndio sababu ya mimi Kupambana usiku na mchana ili kuhakikisha unapata furaha ambayo uliikosa kwa muda mrefu.


"Happy Birthday Mom,Mwenyez Mungu akupe Maisha marefu yenye Furaha,Afya na Amani @mama_dangote," ameandika Diamond Platnumz.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad