Ukweli Kuhusu ‘Bodaboda’ Aliyekuwa Akiyaelekeza Magari Kupita Barabara ya Vumbi





Siku chache zilizopita, video iliyozua gumzo kubwa ilikuwa ikisambaa kwa kasi, ikimuonesha mtu aliyetajwa kama bodaboda, akiyaongoza magari kutoka kwenye barabara ya lami na kupita kwenye barabara ya vumbi.

Wengi waliochangia maoni yao kwenye video hiyo, walikuwa wakicheka na kuonesha kuwa bodaboda huyo aliamua kuwachezea akili watu wenye magari yao kwa kubadilisha pikipiki yake ifanane na zile za polisi kisha kuwapitisha kwenye barabara ya vumbi, akijifanya kuwa ni askari wa usalama barabarani.

Hata hivyo, ukweli kuhusu video hiyo umejulikana.

Jamaa anaitwa George Nyaga, ni balozi wa usalama barabarani nchini Kenya, akiwa pia mwanzilishi wa Chama cha Road Safety Volunteers (RSV) ambacho kazi yake ni kutoa msaada kunapotokea ajali za barabarani kwa kujitolea.


Imeelezwa kuwa video hiyo ilirekodiwa mwaka 2021 na katika eneo hilo, kulikuwa na ajali, hivyo ili kuzuia foleni, akawa anawaelekeza madereva kutumia barabara ya mchepuko (diversion) ili wasikwame kwenye eneo ilipotokea ajali.

Baada ya ukweli huo, watumiaji wengi wa mitandao, wamempongeza Nyaga kwa moyo wake wa kujitolea anaouonesha, ikiwemo kuokoa majeruhi kwenye ajali na kuwawahisha hospitali kwa kushirikiana na wanachama wengine wa chama hicho cha kujitolea.

Unaambiwa jamaa anafanya kazi kuliko hata trafiki! Mwamba apewe maua yake!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad