UKWELI Mchungu: Miquissone, Chama, Kisinda ni Mfano Halisi wa Wachezaji Waliofeli

UKWELI Mchungu: Miquissone, Chama, Kisinda ni Mfano Halisi wa Wachezaji Waliofeli


Tuisila Kisinda, Clatous Chama na sasa ni Jose Luis Miquisone wote wamefeli na njia yao ya kurudi ni kule walipoimbwa. Namna ambavyo warabu hawakutaka kumvumilia Chama azoee mfumo au Kisinda au Miquisone ndivyo ambavyo sisi tunawafanyia wazawa na kuwatukuza wageni. Sisi tunafanya Kinyume.


Wenzetu wanaamini Mgeni kaja kuongeza kitu, wenzetu wanaamini mgeni anastahili nafasi moja tu, nafasi mbili au tatu na malezi ya saikolojia ni kwa wazawa sababu kuna maslahi ya Taifa ndani yake. Kuna kitu nataka watu wa Mpira wa Tanzania wanielewe, wanapaswa kujua ni nini maana ya Kijana wetu, nini maana ya uzao wetu.


Siwachukii wachezaji wa Kigeni, siwachukii hata kidogo nachochukia ni namna tunawalea na namna tunawapa presha wazawa, wageni wanapewa nafasi mbili mbili. Yaani kwa mfano Samatta angefeli Mazembe Simba wangempotezea, Msuva angefeli Difaa Yanga wangempotezea. Lakini Chama, Miquisone na Kisinda wote wamefeli lakini wamepewa nafasi.


Sio Kama wazawa hawajitumi, wanajituma sana ila wanasimangwa sana, wanaombewa sana wafeli kuliko kufaulu. Inafika Kipindi hata timu ya Taifa ina mizengwe juu ya Vijana wetu, inaumiza sana kuona namna tunawafanyia vijana wetu, hatuwapi nafasi ya kuwalea wala nafasi ya kuwakuza badala yake tunawapa nafasi kwa masimango.


Wazawa tunawatumia kama silaha tu ya kumkomoa mpinzani na sio kwa maendeleo ya Taifa wala maendeleo ya kijana. Ikitokea mzawa kadaii haki yake basi ataitwa kila jina baya na dunia nzima itaaminishwa huyu ni mbaya lakini muda utafika tu, watatuelewa tu. Mfano huyu Morrison, alichokifanya yanga kipindi kile angekua mzawa asingesalimiwa.


Anachokifanya Chama muda huu kingefanywa na mzawa tungeambiwa anatumika kuhujumu timu msimu ujao. Fei Toto alitumiwa watu wa kila aina kumtusi na kumuita muhaini wa nchi kisa alikua anadai haki yake ya kimsingi ya kuondoka kwenye mikono ya viongozi wasioona thamani yake. Huyu Chama angekua mzawa mngesikia meeengi.


Tuweke Maslahi ya Vijana wetu mbele kwa maslahi mapana ya Taifa hili, hivi vilabu vikubwa sio haki ya wageni bali liwe daraja kwa wazawa kupepea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad