Upelelezi Kesi Anayedaiwa Kumuua, kumchoma Moto mke Wake Wakamilika

 

Upelelezi kesi anayedaiwa kumuua, kumchoma moto mke wake wakamilika

Mashahidi 28 na vielelezo 14, vinatarajiwa kutolewa mahakamani katika kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Hamis Luongo (41).

Luongo anadaiwa kumuua mke wake aitwaye, Naomi Marijani, tukio analodaiwa kulitenda Mei 15, 2019 eneo la Gezaulole, Wilaya ya Kigamboni, ambapo inadaiwa kuwa baada ya kumuuua alimchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa.

Hayo yameelezwa leo, Juni 30, 2023 na Wakili wa Serikali, Mosie Kaima Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya Mashahidi na Vielelezo (Commital Proceedings) baada ya upelelezi wa shauri hilo kukamilika.

Kaima amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Ramadhani Rugemalira, kuwa upande wa mashtaka unatarajia kuwa na mashahidi 28 na vielelezo 14 zikiwemo nyaraka mbalimbali.

Mshtakiwa baada ya kusomewa maelezo hayo, mahakama hiyo imeihamishia kesi hiyo Mahakama Kuu, kwa ajili ya usikilizwaji wa ushahidi.

Hii ni mara ya pili kwa mshtakiwa huyo kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo, kwani Machi 2021, Luongo alisomewa Commital Proceedings na kesi yake kuhamishiwa Mahakama Kuu.

Hata hivyo, Oktoba 2022 Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) alimfutia kesi na kisha kumfungulia kesi nyingine yenye shitaka la mauaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad