Waarabu wa AL Hilal Kufuru...Sasa Wamtaka Mbappe Kwa TSH Bilioni 812



Klabu ya Paris Saint-German imeruhusu Al Hilal ifanye mazungumzo na mshambuliaji #KylianMbappe baada ya kuweka mezani dau hilo ikiwa ni siku chache zimepita tangu itume barua ya kuhitaji saini ya nyota huyo

Mbappe aliyebakiza mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia #PSG, amedaiwa kutotaka kuongeza Mkataba Klabuni hapo, kitendo kilichotafsiriwa kuwa yuko tayari kuondoka huku akitajwa huenda akajiunga na #RealMadrid

Hata hivyo, licha ya dau hilo, Mbappe hajazungumza lolote au kuonesha kama ana mpango wa kwenda kucheza katika Ligi ya Saudi Arabia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad