Wafumaniwa Wakifanya Ngono Kanisani, ibada zasitishwa

Wafumaniwa wakifanya ngono kanisani, ibada zasitishwa


Kundi la waumini wa Kanisa la Bungonya lililoko wilayani Kayunga nchini Uganda, wamesusia shughuli za ibada baada ya watu wawili kufumwa wakifanya mapenzi ndani ya kanisani hilo.


 Jumanne Julai 5, 2023, saa 2 usiku, mwanaume huyo (23), anayedaiwa kuwa mwanandoa na baba wa watoto wawili, alifumwa na mwanamke ambaye alitalakiwa na mumewe siku chache zilizopita na kulazimika kuishi kwa bibi yake katika kijiji hicho.


Tukio hilo la kushtusha, liliibuliwa na mke wa ndoa wa mwanaume huyo ambaye baada ya kumkuta mumewe akifanya mapenzi ndani ya kanisa alipiga kelele iliyowafanya waumini kujaa na kuwakamata watu hao wakiwa utupu.


Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda, tukio hilo limewafanya viongozi wa kanisa hilo kuingia katika mfungo na maombi yasiyokuwa na ukomo ili kukemea kitendo hicho walichokitaja kama "Dhambi ya kushtusha".


Mwenyekiti wa Mtaa wa Bungonya lilipotokea tukio hilo, George William Kanda amesema watu hao waliingia kanisani kupitia dirishani kabla ya kuanza kufanya tukio hilo.


"Waliingia kanisani kupitia dirishani kwa sababu mlango ulikuwa umefungwa," amesema.


"Mke wa ndoa wa mwanaume huyo alipowafumania alipiga kelele, watu wakajaa kanisani na kuwakamata kisha kuwaleta ofisini kwangu. Mtandio wa kichwani na fulana (t-shirt) ya mwanaume vimehifadhiwa kwa mwenyekiti kama udhibitisho," amesema Kanda.


Kanda aliongeza kuwa baada kufikishwa walihojiwa kisha kuachiwa, huku kesi hiyo ikitarajiwa kuendelea kusikilizwa.


Ofisa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai katika Wilaya ya Kayunga nchini humo, Beatrice Ajwang pamoja na kukiri kusikia tukio hilo, amesema hakuna kesi iliyowasilishwa ofisini kwake.


Kiongozi wa Kanisa la Bugonya Uganda, Aaron Komugisha amesema kanisa limeandaa ibada itakayokutanisha viongozi wa kanisa wilayani humo kuliombea kanisa na kuliweka wakfu kabla ya shughuli za ibada kurejea.



"Viongozi waliotembelea kanisa hili walishtushwa na kitendo hicho," amesema Aaron.


"Watu hao wanatakiwa kutubu dhambi zao mbele ya Mungu," amenukuliwa mmoja wa shuhuda wa tukio hilo.


Kijiji cha Bugonya kipo takribani Kilometa 35 kutoka mjini Kayunga.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad