Wakili Madeleka Akamatwa na Polisi Arusha

 

Wakili Madeleka Akamatwa na Polisi Arusha

Wakili wa Kujitegemea nchini, Peter Madeleka amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha katika Kituo Jumuishi cha utoaji hai mara baada ya kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.


Madeleka amekamatwa muda mfupi baada ya kujifungia kwa zaidi ya dakika 30 katika chumba cha Mahakama hiyo cha Jaji Aisha Bade ambaye ndiye alitoa maamuzi katika kesi yake ya kupinga makubaliano ya kukiri kosa kati yake na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka (DPP).


Kabla ya kukamatwa Wakili Madeleka kupitia akaunti yake ya Twitter leo Jumatatu aliandika kuwa maofisa wa Jeshi la Polisi wanamuwinda nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ili wamkamate baada ya kufutiwa Plea Bargaining na Jaji Bade.


Plea Bargaining hiyo ilitokana na kesi ya uhujumu uchumi iliyotolewa uamuzi Aprili 27 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambapo wakili Madeleka alihukumiwa kulipa faini ya Sh. 200,000 au kutumikia kifungo cha nje cha miaka mitatu.


Hata hivyo katika uamuzi huo alilipa Sh. Milioni 2 kwa DPP ili kuondolewa shauri hilo baada ya kulazimika kukiri makosa.


Leo Jumatatu akiwa mahakamani, Wakili Madeleka aliandika ujumbe kuwa “Hukumu iliyosomwa leo na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha mbele ya Jaji Bade licha ya kufuta Plea Bargain kati Madeleka na DPP, ilikuwa imeshajulikana kwa polisi na DPP kabla ya kusomwa na mahakama ikasaidia mazingira ya mimi kukamatwa,”


Dakika chache baadae Wakili wa Madeleka katika mahakama hiyo, Simon Mbwambo na wanahabari wakili Madeleka alitoka ndani ya chumba cha mahakama na kukamatwa na polisi.


Wakili wa Madeleka, Mbwambo amesema hajui kosa la mteja wake Zaidi ya kuwaona polsi wakimkamata na kumpeleka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad