Wakili Nshala Aliyewahi Kuwa Rais wa Aitwa Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kisa Bandari



Dk. Rugemeleza Nshala
WAKILI Rugemeleza Nshala aliyewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ameitwa na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam leo tarehe 11 Julai 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa jana tarehe 10 Julai 2023 kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ilimtaka wakili huyo kufika katika ofisi hiyo kutokana na kauli alizozitoa tarehe 3 Julai 2023 na kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Tarehe 3 Julai 2023, Dk. Nshala alitoa maoni ya kupinga makubaliano yanayohusu uwekezaji, uendelezaji na uendeshaji wa bandari uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai akieleza baadhi ya vifungu vinapingana na Katiba ya nchi.

Pia wakili huyo alidai kutishiwa kuuawa bila kufafanua ni vitisho vya namna gani hata hivyo alijinasibu kuwa yupo tayari kufa kwa kulitetea Taifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad