Walichokisema Yanga Baada ya Kupangiwa na ASAS FC Ligi ya Mabingwa CAF


Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema malengo ya chini katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika inayotarajiwa kuanza mwezi ujao ni kutinga hatua ya makundi

Katika droo ya mechi za awali na raundi ya kwanza ambayo ilifanyika jana huko Misri, Yanga imepangwa kuanzia Djibout kuikabili Asas Fc

Mechi ya mkondo wa kwanza itapigwa kati ya August 15-20 na mechi ya marudiano itapigwa wiki moja baadae jijini Dar es salaam

Kama Yanga itafanikiwa kufuzu hatua ya awali kwenye raundi ya kwanza itacheza dhidi ya mshindi wa mechi kati ya Otoho Fc ya Congo dhidi ya Al Marreikh ya Sudan

Katika raundi ya kwanza pia Yanga itaanzia ugenini na kumalizia mechi ya pili nyumbani

Kamwe amesema wanajiandaa kwa mechi hizo na jambo muhimu ni kuwaheshimu wapinzani wao


"Sisi kama Yanga Africans tumeipokea vizuri droo iliyopangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika. Nataka niwaambie Wanachama na mashabiki wetu kuwa hakuna timu ndogo kwenye Ligi ya Mabingwa, kila timu inajiandaa ili kuweza kufanya vizuri"

"Tuna muda mrefu sana hatujacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika. Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwetu tukifanikiwa kucheza fainali ya kombe la Shirikisho la CAF. Msimu huu malengo ya klabu ni kuona kwanza tunatinga hatua ya makundi"

"Nawaomba Wanachama na Mashabiki wetu tuhamishe nguvu zetu kwenye michuano hii, tuhakikishe tunacheza hatua ya makundi," alisema Kamwe

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad