Wapinzani wa Simba na Yanga Ligi ya Mabingwa Afrika Hawa Hapa



Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limeendesha draw ya kutambua timu zitakazokutana kwenye hatua za awali za Kombe la Klabu Bingwa (CCL).

Klabu ya @yangasc imepangwa kucheza na klabu ya ASAS ya Djibouti katika hatua ya kwanza ya mtoano Ligi ya Mabingwa Afrika. Na mshindi kati yao atakutana, kati ya AS Otohô ya nchini Congo au El Merrick ya Sudan.

Kwa upande wa @simbasctanzania wao wataanzia mzunguko wa pili. Kwa hiyo itacheza na mshindi kati ya African Stars ya Namibia na Power Dynamos ya Zambia, katika kuwania kufuzu hatua ya makundi.

Huwenda Mnyama akakutana na Power Dynamos mara mbili ndani ya mwaka huu kwani wamewaalika pia kwenye kilele cha 'SIMBA DAY' Agosti 6.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad