Watatu Wajeruhiwa Vibaya Ajali Mikumi





AJALI mbaya imetokea leo majira ya saa 9 usiku katika barabara inayopita katikati ya Hifadhi ya Taifa Mikumi, mkoani Morogoro na kusababisha majeruhi watatu ambao wamewahishwa katika Hospital ya Senti Kizito Mikumi, hakuna kifo.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Noah yenye namba za usajili T 361 DMG, na fuso, na kwa mujibu wa dereva wa fuso Edwardi Chura, chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Noah aliedai kuwa alikuwa anasinzia jambo lililosababisha kugonga lori na kupoteza muelekeo na kwenda kugongana uso kwa uso na fuso hilo na kupinduka.

Imeelezwa kuwa Noah hiyo ilikuwa inatoka muelekeo wa Mikumi kwenda Dar es Salaam na fuso lilikuwa linatoka muelekeo wa Morogoro mjini kwenda Iringa, ambazo baada ya kugongana ziliziba njia na kusababisha foleni kubwa iliyodumu kwa takribani saa tatu.

Dereva Chura, amesema wao hawakupata majeraha zaidi ya gari yao kuumia, na kwamba walioko kwenye Noah ndio waliojeruhiwa vibara akiwemo dereva ambaye alivunjika miguu yote na mkono.

"Baada ya kupata ajali tulitoka na kwenda kusaidia kuwatoa walioko kwenye Noah, lakini tulikaa zaidi ya saa mbili ndio tukapata msaada, na asilimia kubwa watu watatu kati ya watano waliokuwemo kwenye Noah waliumia vibaya," amesema Chura.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad