Waziri Angellah Kairuki Atoa Maagizo Matatu Kutatua Kero za Waalimu

 

Waziri Angellah Kairuki Atoa Maagizo Matatu Kutatua Kero za Waalimu

 

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angellah Kairuki amewaagiza maofisa utumishi na makatibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), kuhakikisha wanafuatilia walimu ambao hawajapandishwa vyeo kwa muda mrefu.


Maagizo mengine ni kuhakikisha kuwa madai ya walimu wote ikiwemo malimbikizo ya mishahara yanaingizwa katika mamlaka husika na kufuatilia madai ya malimbikizo ya fedha za likizo na uhamisho.


Kairuki ametoa maagizo hayo leo Jumatano Julai 5, 2023 wakati akifungua kikao cha maofisa utumishi wa wilaya na makatibu wa TSC wa wilaya zote Tanzania Bara.


“Naomba muende mkawe na mawasiliano mazuri katika utendaji wenu wa kazi ikiwemo kutumia lugha za staha kwa walimu pale wanapoleta changamoto zao,”amesema.


Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi, Dk Charles Msonde amesema walifanya utekelezaji wa maagizo ya kutatua changamoto za walimu ikiwa ni pamoja na kuunda kikosi kazi cha kuwasikiliza.


Amezitaja changamoto hizo ni upandishaji wa madaraja, kupishana kwa muda wa kupandishwa madaraja bila utaratibu na mfumo wa kubadilishwa vyeo cheo.


Katibu Mtendaji wa TSC, Paulina Mkwama ameishukuru Serikali kwa kutoa vitendea kazi ikiwemo magari 16 na kompyuta 159 kwa watendaji wa Tume hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad