Yanga Hawataki Mchezo, Mchezaji Bora MVP wa Ivory Coast, Pacome Zouzoua Atambulishwa Jangwani

 

Yanga Hawataki Mchezo, Mchezaji Bora MVP wa Ivory Coast, Pacome Zouzoua Atambulishwa Jangwani

Klabu ya Yanga SC imekamilisha Usajili wa Kiungo Mshambuliaji fundi wa Kimataifa wa Ivory Coast na Klabu ya ASEC Mimosas, Zouzoua Pacome 'Zinadine Zidane' kwa Mkataba wa Miaka miwili.


Taarifa iliyotolewa na Yanga imeeleza;


Kuna usajili, halafu kuna usajili mkubwa. Wanachofanya uongozi wa Young Africans Sports Club kwenye dirisha hili la usajili, ni kufanya usajili mkubwa.


Ilianza kwa Nickson Kibabage, Jonas Mkude, Gift Fred, Yao Kouassi, Maxi Nzegeli, akaja Skudu, na leo uongozi wa Mabingwa wa Kihistoria Nchini umekamilisha usajili mkubwa wa kiungo Pacome Zouzoua kutoka Asec Mimosas.


Kiungo huyo wa Kimataifa kutoka Ivory Coast amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.


Pacome ameondoka Asec akiwa na rekodi ya kuwa mchezaji bora wa kikosi hiko na akifanikiwa kushinda tuzo ya Mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu ya Ivory Coast ‘MVP’ msimu wa 2022/23.


Ndani ya msimu wa 2022/23, Pacome aliyeanza maisha yake ya soka kwenye timu ya vijana ya Sparta Prague ya Jamuhuri ya Czech, amefunga mabao 7 na kutoa Asisti za mabao 4.


Vilevile, Pacome amepita kwenye timu tofauti tofauti ikiwemo, SC Gagnoa, Daugavpils, Africa Sports kabla ya kutua Asec Mimosas msimu wa 2021/22.


Msimu uliomalizika, Pacome alikua MVP [Mchezaji Bora] wa Ligi kuu ya lvory Coast na MVP wa Klabu yake ya Asec Mimosas Akiwazidi Aubin Kramo (amesajiliwa Simba Sc) na Mohamed Zoungrana (anakaribia kusajiliwa USMAlger).


Ni kiungo Mshambuliaji [Namba 10] ambaye alifunga mabao saba [7] na assist nne [4], Tuzo ya MVP ilimfanya akabidhiwe gari ya kutembelea kupitia mfuko wa Frank Kessie.


Pacome Zuzwa anaweza kuongeza nguvu kwenye nafasi ya Stephanie Azizi KI, yani namba 10, itategemea na Gamondi ataamua nini.


Usajili huu unakua watatu kwa wachezaji kutoka klabu ya Asec Mimosas kwa ajili ya msimu ujao wa 2023/24 Alianza Atohoulla Yao na Kramo Aubin.


Miongoni mwa mabao safi aliyofunga ni lile ambalo beki aa kulia Atohoulla Yao (amesajiliwa Yanga pia) alimpigia cross Pacome Zouzou na kuzamisha wavuni. wakiwa Asec. Wote ni Jeshi la Wananchi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad