Yanga yakwepa rungu Fifa ikimalizana na Eymael Luc

 

Yanga yakwepa rungu Fifa ikimalizana na Eymael Luc



MASHABIKI wa Yanga walikuwa na presha juu ya timu yao kupewa kibano cha kuzuiwa kusajili madirisha matatu kutokana na deni ya kocha wa zamani wa timu hiyo, Luc Eymael, hata hivyo mabosi wa klabu hiyo wamekwepa kijanja rungu la Fifa kwa kuamua kumzalizana na kocha huyo.


Kocha Eymael amethibitishwa kumaliziwa sehemu ya fedha alizokuwa akiidai Yanga kwa kumvunjia mkataba mwaka 2020 na kusababishwa klabu huyo kuwa hatarini  kufungiwa kusajili kwa madirisha  matatu kulingana na taarifa ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).


Eymael aliiburuza Yanga kwa Fifa kutokana na kuchelewa kumlipa madai ambayo ni zaidi ya dola 66,000 (zaidi ya Sh 159.7milioni) pamoja na riba ya asilimia tano.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji, alisema viongozi wa Yanga walimwekea pesa yake Jumapili iliyopita pamoja na riba elekezi, hivyo kiwango kilichosalia ni asilimia chache mno;


"Robo tatu ya pesa wanazotakiwa kunilipa wamenipa, nashukuru kwa hilo kwa sababu nataka tumalizane kwa amani," alisema Eymael


"Hayo mambo ya kufungiwa sio kitu ambacho napenda kwa sababu nilikuwa na wakati mzuri Tanzania ni vile tu kulitokea changamoto za hapa na pale ambazo zilichochea kushindwana, inabidi maisha meingine yaendelee."


Kwa upande wake Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema wamemwekea mzigo wake kocha huyo hivyo hakuna uwezekano wa kufungiwa; "Tupo bize na mipango yetu ya usajili kwa sasa, tumeshamwekea hela zake."


Kama Yanga ingeshupaza shingo kwa mujibu wa FIFA wangekumbana na rungu la kufungiwa vipindi vitatu vya usajili pamoja na kuondolewa kwenye michuano ya kimataifa ambayo watashiriki msimu ujao wa 2023/24.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad