Young Killer Avuruga Mipango ya Diamond Platnumz, Amshusha Namba Moja Trending


Rapper @youngkillermsodokii ni kama amevuruga mipango ya msanii @diamondplatnumz aliyokuwa amejiwekea ya kukaa namba moja kwenye Trending YouTube kuanzia Julai hadi ifikapo Januari 2024.

Kupitia Freestyle Session 6 ya Msodoki iliyoachiwa Julai 10, ambayo amemchana rapper @younglunya imeishusha 'Baby' REMIX hadi namba mbili na yeye kukaa namba moja kwenye nyimbo zinazofanya vizuri zaidi Tanzania (Popular Right Now).

Wakati huo huo, Msodoki kwenye Trending (For Music) anashika namba 4 na 'My Baby' bado ipo namba moja huko YouTube huku Freestyle Session 5 ya Lunya ikiwa namba tatu.

Huwenda @diamondplatnumz akarejea tena namba moja kwenye nyimbo zinazofanya vizuri zaidi Tanzania (Popular Right Now) YouTube kupitia mikwaju yake hiyo ambayo bado inafanya vizuri.

Mapema leo asubuhi @diamondplatnumz ameachia video ya wimbo wake 'Shu' aliomshirikisha @chley_nkosi lakini pia nikukumbishe kuwa wawili hawa miaka minne iliyopita walishirikiana kwenye ngoma iitwayo 'Pamela'.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad