Zamaradi Apinga Vikali Mume na Mke Kufichana Password za Simu Kwenye Ndoa


Tunapozungumzia simu kushikwa pia hatumaanishi ndio PATROL mtu akiingia tu haya leta simu, Hapana😄

Maana inayosemwa hapa ya kushika simu ni kila mtu kuwa na uhuru wa simu ya mwenzake inapobidi bila kuhojiwa, Kama zina password binafsi sioni kama ni Sahihi hasa kwa MUME NA MKE kutokujuana password za kila mmoja!! SIMU NDIO MAISHA,na mmeamua maisha yenu kuyatumia pamoja, ni nini kikubwa ambacho usingependezwa mwenzi wako akifahamu!!!?

MSINGI WA KWANZA wa ndoa kabla ya yote ni KUAMINIANA!!! Kuaminiana sio kuachiana tu kama Mbuzi isiyo na mchunga ila ni kuachiliana mioyo na kuamini niko salama kwenye mikono ya mwenza wangu, Ndoa ni pale wawili wanapokuwa mwili mmoja, mnapokuwa wamoja mnaunganisha familia, hakuna jambo la AIBU tena kati yenu, kama shida za ukoo ni zenu wote, maana hata utatuzi mtasaidiana, kama ni matumizi yako wazi, hakuna mtu anasaidia kwao kwa uficho, hivyo SABABU YA KUSEMA KUNA MAMBO YA FAMILIA AMA SIRI ZA OFISI ni janja janja tu ya kukwepa 😆

Kama mmeoana kweli Ndoa na sio kuingia KUJARIBU basi hakuna Siri baina yenu, SABABU YA SIRI ITAKUWA MUHIMU PALE TU UNAPOSHIRIKI NA MTU MWINGINE KUFANYA UNAYOTAKIWA KUFANYA NA MKEO AU MUMEO 😆😆
kama lengo ni moja SIRI HAITAKUWEPO ila kama ni ndoa za kuviziana ofcourse weka siri, nanunua hiki sitaki huyu ajue, nina Abdallah au Rose nje nachat nae ananifurahishaga tu sitaki mke wangu aone, tayari umekiuka’ ukiona kitu mtu hutaki aone ujue hakifurahishi 😁,Na hata ukiona kitu wewe huko tayari kuona ujue kina dalili za kutisha😁

Nyinyi ni mwili mmoja, Simu unaogopea nini!? Aidha humuamini au HUJIAMINI kinyume na hapo hakuna kingine, labda kama una kazi ya hatari ambayo unaogopa jamii yako isijue (tatizo pia)

Na hata kama ana tabia zake mbaya basi asiwe na UHURU MKUBWA WA KUZISHIRIKI kiasi amekaa na wewe pembeni anachat kwa uhuru ila kwakuwa simu kila mtu na yake hana shaka, ndio ile mtu yuko na mkewe ila mchepuko muda wote akimtaka anampata kwa msg na maisha yanaendelea 😁’ hata heshima inakuwa haipo, kucheat tu hata kisiri sio heshima, sasa basi isifike hata kucheat kwenyewe Haogopi tena, ANACHEAT KWA AMANI 😆

Haiwezi ikawa kila mtu na maisha yake kama kweli mmeamua kuishi pamoja😊

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad