Ziiki Waendelea Kulaumiwa na Wasanii, MB Dogg Ajitokeza Adai Wamemdhulumu Pesa Kwa Miaka 13 , Diamond Ahusishwa


Mwimbaji wa Bongo Fleva, MB Dogg ameendelea kupaza sauti lengo ikiwa ni kutaka kupata Haki yake ambayo ameikosa kwa takribani miaka 13.

Kwa mujibu wa andiko la mkali huyo wa 'Si Uliniambia', ameitaka kampuni ya Ziiki Media ya Afrika Kusini na Msanii @diamondplatnumz ambaye anadaiwa kuwa sehemu ya wamiliki wamlipe pesa zake zitokanazo na matumizi ya kazi zake bila ridhaa yake.

"Ziiki Media kwa niaba ya Naseeb Abdul Juma Issack, nahitaji pesa zangu mlizochuma kwa miaka 13. Hata kama ni Shilingi Mia ni Haki yangu".

Baada ya @mbdogg_master kufanya uchunguzi alibaini kuwa mapato yanayotokana na nyimbo zake yanachukuliwa na Kampuni hiyo bila ruhusa wala kuwa na makubaliano ya kimkataba na msanii husika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad