Aggy Amvaa Kajala: Mama Unavaaje nguo ya Ndani Mbele na Mkwe wako?

Aggy amvaa Kajala: Mama unavaaje nguo ya ndani mbele na mkwe wako?

 

Msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Agness Suleiman maarufu kama Aggy Baby amesema kuwa msanii mwenzake, Kajala Masanja anaishi maisha ambayo si ya Kitanzania.


Aggy anasema; "Kumzungumzia Kajala ni kitu cha kawaida kwa sababu ana maisha flani siyo ya Kitanzania. Yale maisha ya Kajala, Paula na Marioo yanashangaza, kwanza mzazi huwezi kuvaa chup* mbele ya mkwe, Watanzania hatuna desturi hiyo kabisa, halafu ana maisha ambayo Watanzania hatuishi na siyo tamaduni zetu.


"Kwa hiyo tukiona vile vitu lazima tuvizungumzie tuvikataze, labda kama Kajala aseme yeye siyo Mtanzania hapo tutaacha kuongea, lakini kama yeye ni Mtanzania na tunaona kwamba anapotosha jamii, anapotosha jinsi watu wanavyotakiwa wamuone yeye kama msanii.


"Lazima tuongee aache kupotosha jamii, yeye ni mama mtu mzima ana mtoto ambaye nae ameshakuwa mtu mzima sasa unapigaje picha za uchi wakati ile ni stara ya kwako wewe na mume wako ndani, lakini anajiachia na mkwe anaona, anataka mkwe aone nini," amesema Aggy Baby.


Lakini pia Aggy amezungumzia kitendo cha Aunty Ezekiel kutumia picha ya uchi ya Kajala kumuwishi katika siku yake ya Birthday, ambapo anasema ule ni unafiki na udhalilishaji.


"Mimi nafikiri wanaishi kinafiki kwasababu hakuona picha nyingine za kuposti mpaka amposti mwenzake picha ambayo inamuonyesha maungo yake yote, kwahiyo anamsambazia watu waone jinsi ambavyo akili ya Kajala haiko sawa.


"Kwa sababu kuna kitu kinaitwa afya ya akili, huwezi posti picha ambayo siyo desturi yetu ukaacha picha ambazo amevaa vizuri amependeza, kwahiyo wanaishi kinafiki, sioni kama kuna mapenzi kati yao wawili," amesema Aggy Baby.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad