Aggy Baby: Mahari Sh Mil 500, Wanaume Wameminika Kutaka Kunioa

 

Aggy Baby: Mahari Sh Mil 500, Wanaume Wameminika Kutaka Kunioa

 Aggy Baby: Mahari Sh Mil 500, Wanaume Wameminika Kutaka Kunioa

Msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Agness Suleiman maarufu kama Aggy Baby ametusanua kuwa maelfu ya wanaume wameminika wakituma maombi kwake kutaka kumua lakini ameweka vigezo ili kumpata mume anayemhitaji.


Hatua hii ya Aggy inakuja baada ya staa huyo kutangaza kuwa kwa mwanaume yeyote mwenye ndoto ya kumuoa basi ahakikishe ana kibunda cha Tsh milioni 500 kwa ajili ya kumtolea mahari, vinginevyo kaa pembeni.


Aggy anasema; "Baada ya kutangaza mahari ya Tsh milioni 500 ili kunioa, wamejitokeza wanaume wengi lakini sasa kwenye kuchagua ndio mtihani, maana lazima niwafanyie interview, pamoja na kwamba una hizo Tsh milioni 500 lakini lazima nikufanyie interview kama unaweza vile vitu vyangu vingine navyovitaka.


"Kwanza lazima nikuulize una kiasi gani kwenye akaunti yako? Kuachana na Tsh milioni 500 ambazo utanipa, swali la pili nawauliza, je, ukiwa na mimi unaweza kunifulia, kunipikia na kufanya shughuli zangu za ziada?


"Swali la tatu sihitaji kuzaa, kama anaweza kunioa basi hakuna watoto, mimi sina muda na sihitaji watoto, akitaka nimzalie lazima anilipe pesa nyingine kwa ajili ya kumzalia mtoto," amesema Aggy Baby.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad