Ahmed Ally "Niweke Wazi Huu Mwaka ni Wetu Wana Simba"


Ahmed Ally "Niweke Wazi Huu Mwaka ni Wetu Wana Simba

Mechi ya fainali [Ngao ya Jamii] tulikuwa tunaitaka sana, akili zetu zilikuwa zinaifikiria hiyo fainali lakini tulijua kufika fainali ni ngumu kwa sababu ya ugumu wa mpinzani ambaye tulikuwanae kwenye hatua ya nusu fainali.

Tumefanikiwa kuvuka nusu fainali sasa tunakwenda kwenye jambo ambalo kimsingi limetuleta hapa Tanga.

Mechi ambayo tunaitaka sana ni dhidi ya Yanga, sina kumbukumbu kama Simba na Yanga zimewahi kucheza uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Niweke wazi kuwa huu ni mwaka wetu na tunahitaji kuandika historia nzuri ndani ya Mkwakwani, Tanga.

- @ahmedally_, Meneja Habari na Mawasiliano Simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad