Alex Ngereza Aongea Ukweli Mchungu: Dickson Job Ameanza Kupotea, Kimo Chake Kinamponza

 

Alex Ngereza Aongea Ukweli Mchungu: Dickson Job Ameanza Kupotea, Kimo Chake Kinamponza

 Alex Ngereza Aongea Ukweli Mchungu: Dickson Job Ameanza Kupotea, Kimo Chake Kinamponza

Beki Bora wa msimu uliopita Dickson Job hajaonekana katika michezo mitatu ya Yanga waliyocheza mpaka sasa chini ya mwalimu mpya Miguel Gamondi.


Badala yake Muargentina huyo amekuwa akiwapa nafasi Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca.


Sasa Mchambuzi wa Michezo kutoka TV3 Alex Ngereza ametudokeza sababu hasa za mlinzi huyo kutopata nafasi ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;


"Taratibu taratibu beki bora wa msimu uliopita Dickson Job ameanza kupotea kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga inawezekana kimo chake ndio kinasababisha Migue Angel Gamondi hampi nafasi kwenye kikosi cha kwanza


Makocha wengi kutoka Ulaya na America wanapenda kutumia mabeki warefu ndio maana Bacca na Bakari Nondo Mwamnyeto wanatumika zaidi kuliko yeye"


Je ndio mwisho wa utawala wa Job Yanga? tupe maoni yako

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad