Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wachezaji na benchi la ufundi wanastahili pongezi kwa kucheza mechi nne ndani ya siku 12 na kuweza kushinda zote
Ahmed amesema ni shauku ya Wanasimba kuona timu yao ikicheza soka la kuvutia maarufu 'pira biriyani', lakini jambo muhimu kwanza ni kuhakikisha timu inashinda mechi zake hivyo kocha Robertinho Oliveira ameanza kutengeneza timu ya ushindi kwanza
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Ahmed ameandika ujumbe huu;
"Wachezaji wetu na Benchi la Ufundi wanastahili pongezi, wamecheza 4 ndani ya siku 12 na zote wamepata ushindi
Kwa interval hiyo usitegemee timu kucheza kwa kiwango kikubwa sana bali ni kucheza kwa malengo
Pamoja na hayo kikosi chetu kina wachezaji wapya 11, ni ngumu mno timu yenye maingizo mapya kucheza kwa maelewano makubwa
Kwa kufahamu hilo Mwalimu Robertinho ameanza kwanza kutengeneza timu ya ushindi baada ya uhakika wa ushindi ndipo atageukia mpira mzuri
Kwenye kuhakikisha timu inapata kwanza ushindi, Mwalimu anatumia zaidi Wachezaji wa zamani huku wale wapya akiwapa nafasi mmoja baada ya mwingine
Wana Lunyasi tuendelee kuwa na imani na Mtaalamu Robertinho na tumpe muda wa kufanya kazi yake
Kutengeneza Pira Biriani inahitaji sana muda
Ukitaka kuamini kucheza pira biriani sio jambo dogo kuna watu hawajawahi kucheza mpira huo tangu kuumbwa kwao"