Baada ya Kuanza Kutupia SIMBA, Moses Phiri Atangaza Hatari Kwa Mabeki Wote
MSHAMBULIAJI wa Simba, Mosses Phiri ametangaza hali ya hatari kwa mabeki wa timu pinzani kwa msimu huu kwa kufunga mabao zaidi akiendelea kupata nafasi ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa msimu wa 2023/24 wa mashundano ikiwemo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika mchezo wa juzi Phiri aliingia dakika ya 53 na kufunga bao lake la kwanza katika mechi yake ya pili ya Ligi hiyo akiingia uwanjani kuchukuwa nafasi ya Jean Baleke, dhidi ya Dodoma Jiji FC, uliopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Nipashe jana mara baada ya kukamilika dakika 90 za mchezo huo, Phiri alisema amefurahi sana kufunga bao lake la kwanza kwenye mechi hiyo.
Alisema anafikiria kuendelea kufunga zaidi kila anapopata nafasi ya kucheza na kufanya kile aluchokifanya msimu uliopita kwa kufunga idadi ya mabao 10 kabla ya kupata majeraha.
“Nafurahi kucheza mechi yangu ya kwanza na kufunga bao , ninaimani kwa kushirikiana na wenzangu nitawapa furaha mashabiki wa Simba na kuhakikisha tunapambana kufikia malengo wanayoyatarajia ikiwemo kushinda kila mechi.
“Matarajio yangu ni kufunga zaidi kila ninapopata nafasi ya kucheza, msimu uliopita nilifunga mabao 10 na sikuweza kuendelea kwa sababu ya majeraha ninaimani na kumuomba Mungu kuninalia afya njema ili niweze kukata kiu ya mashabiki wetu,” alisema Phiri.
Aliongeza kuwa hawezi kuahidi atafunga mabao mangapi kwa sababu matarajio yake na wenzake ni kuhakikisha msimu huu mashabiki wao wanapata furaha kwa kupambana kusaka poiti tatu muhimu kwa kila mechi.” Alisema Phiri.