Ommy Dimpoz Akiri Kufunga Ndoa na Mzungu Kutoka Marekani



Ommy Dimpoz amekiri fununu kwamba miezi michache iliyopita alifunga ndoa ya kimyakimya na mwanamke wake wa kizungu raia wa Marekani ambaye walikuwa wapenzi kwa muda kabla ya kuwa rasmi kama wanandoa

"Nilifunga ndoa ya kimyakimya na mke wangu ambaye ni raia wa Marekani na tulikutana hukohuko Marekani" - Ommy ameiambia The Switch ya Wasafi FM

Aidha, Ommy amekana madai yalikuwa yameenea kwamba yeye na marehemu Maya Mia walikuwa wapenzi, amesema yeye na Maya Mia walikuwa marafiki wa kawaida tu, Maya Mia alikuwa mmoja wa professional makeup artist duniani aliyeishi Tanzania na kufanya kazi na makampuni makubwa ya vidozi nchi za mabara tofauti tofauti ingawa alikuwa anatokea nchini Mercedonia

Vilevile katika interview husika na The Switch, Wasafi FM, Ommy Dimpoz amesema kazi yake ya ubunifu(creativity) katika kampuni ya GSM anaifurahia zaidi kuliko hata kazi zake za muziki huku akimshukuru bosi wa GSM kwa kumpa fursa aoneshe uwezo wake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad