BOT yapokea noti zinazodaiwa ‘chuma ulete’



Lindi. Meneja Huduma za Kibenki wa Benki Kuu Kanda ya Kusini, Melchiades Rutayebesibwa amesema fedha zilizochakaa zimekuwa zikirudishwa ili kubadilishwa ambapo zipo zilimwagikiwa rangi, zilizoandikwa na zingine huja zikiwa zimekatwa katika pembe nne.

Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyotokana na maswali aliyoyauliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini alipotembelea katika banda la maonyesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. Alihoji kwanini baadhi ya benki za biashara zinatoa fedha zilizochakaa kwa wananchi.

Amesema kuwa katika mapokezi ya fedha chafu huwa wanapokea zilizomwagikiwa na rangi, zilizochorwa au kukatwa kwenye pembe nne za noti kwa imani za kitamaduni (chuma uletee) na zingine huunganishwa kwa gundi.

"Kuna wakati zinakuja fedha kubadilishwa zingine zinakuwa zimemwagikiwa rangi, zingine zimechorwa au kukatwa kwenye kingo nne za noti zake kwa imani za kitamaduni (chuma uletee)," amesema Rutayebesibwa.


“Unajua moja ya sera ya Benki Kuu ni kuhakikisha wakati wote uwepo wa fedha safi katika mzunguko wa fedha hapa nchini na ikumbukwe Benki Kuu kupitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2006 inawajibu wa kutengeneza pesa za Kitanzania,” amesema Rutayebesibwa.

“Tunazisambaza fedha za Kitanzania hapa nchini kupitia mabenki ya biashara kwa kuondoa fedha zote kwenye mzunguko hapa nchini hasa zilizochakaa ama zilizoharibika au aina yoyote ya uharibufu,” amesema Rutayebesibwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amehoji kwanini BoT wanaruhusu fedha chafu zilizochakaa kutolewa ndani ya benki za biashara," amesema.


“Kuna wakati unachukua fedha katika benki za huko vijijini mpaka unajiuliza hii pesa imetoka benki kweli zipo baadhi ya benki unakuta wanapesa safi mpaka unapenda ukatoe mara kwa kwa mara huko,” amesema Sagini.

“Lakini kuna vibenki huko sijui wakileta mnawapiga faini nahisi ndiyo maana wanaogopa kuleta. Unakuta benki ipo kijijini ukitoa fedha unachanganyikiwa ilivyochafu, wakati sisi tunaamini kuwa fedha ukitoa benki lazima iwe safi,” amesema Sagini. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara, Nassor Omari amesema kuwa huwa wanaweka muda maalumu ambao benki za kibiashara hukusanya na kichambua fedha zilizochakaa na kuzirudisha ambapo hupewa mpya.

“Kabla hawajaleta kwetu wanakaa na kuzichambua ili zilizosafi zinabaki na zilizochakaa zinarejeshwa Benki Kuu ili kupata mpya kama zipo zilizochakaa na wanazitoa kwa wananchi hilo ni tatizo  la benki za kibiashara,” amesema Omary.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad